Simba Sports Club
News

Abdulrazack Hamza ni Mnyama

4 Jul 2024

Abdulrazack ni mchezaji kijana wa Kitanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini kwa ubora mkubwa akiwa kwenye kikosi cha kwanza.

Abdulrazack ana umri wa miaka 21 bado ana nguvu na muda mrefu wa kucheza soka na tunaamini atakuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi chetu.

Ukiacha ubora alionao na umri wake Abdulrazack ni mchezaji ambaye anaijua vizuri Ligi ya Tanzania kwakuwa amecheza kwa ubora katika timu za Mbeya City, KMC na Namungo FC.

Advertisement

Abdulrazack amekuja kuongeza uimara katika idara ya ulinzi wa kati ambapo anakuja kuungana na Che Fondoh Malone na Lameck Lawi.

Abdulrazack anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa kuelekea msimu ujao wa Ligi baada ya Lameck Lawi, Joshua Mutale, Steven Mukwala na Jean Charles Ahoua.

Back to homepage
Share this story