Simba Sports Club
News

13 Wachukua fomu, wanne wautaka uenyekiti

12 Dec 2022

Kati ya wagombea hao wanne wanawania nafasi ya mwenyekiti na tisa nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti ni aliyekuwa Mtunza Fedha wa klabu, Yusuph Nassor Majid ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS).

Wengine wanaowania ni Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Geofrey Nyange 'Kaburu' Yusuph Omar Yenga, na Eng. Rashid Khamsini.

Advertisement

Katika nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi mpaka sasa waliochukua fomu ni wagombea tisa.

Wagombea hao ni Iddy Noor Kajuna, Abubakar Zebo, Eng. Rashid Khamsini, Hawa Subira Mwaifunga, Laurian Mganga, Elisony Edward Mweladzi, Lameck Lawrance na Abdallah Rashid Mgomba.

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litafungwa rasmi Disemba 19, mwaka huu.

Back to homepage
Share this story