Miquissone mchezaji bora wa mashabiki Februari

Kiungo mshambuliaji Luis Miquissone ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Februari ambayo inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile (Emirate Simba Fans Player of the Month).

Pamoja na tuzo hiyo, Miquissone pia amekabidhiwa pesa taslimu Sh1,000,000 kama sehemu ya zawadi.

Miquissone amekuwa kwenye kiwango bora ndani ya Februari ambapo amemshinda beki kisiki Joash Onyango ambaye ameingia naye fainali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Miquissone amesema si tuzo yake pekee bali ni ya wachezaji wote kutokana na ushirikiano wao wa ndani na nje ya uwanja.

“Namshukuru Mungu kwa kufanikiwa kupata tuzo hii, nawashukuru waandaji na wadhamini Emirates Aluminium kwa tuzo hii. Hii ni tuzo ya wachezaji wote wa Simba sababu tunashirikiana,” amesema Miquissone.

Kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo kulikuwa na tukio la kusaini mkataba wa makubaliano kati ya Mwakilishi wa Emirates Aluminium, Issa Maeda na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara ambao utadumu hadi mwisho wa msimu huu.

Mwisho wa msimu kutakuwa na tuzo ya mchezaji bora wa mwaka (MVP) ambapo nyota watano wataingia kwenye fainali ya kinyang’anyiro hicho.

SHARE :
Facebook
Twitter

5 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER