Mgunda akabidhiwa tuzo yake CCM Kirumba

Kocha Mkuu Juma Mgunda amekabidhiwa tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC mwezi Novemba muda mfupi kabla ya kuanza mchezo wetu dhidi ya Geita Gold kuanza katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Mgunda amewashinda makocha Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars na Meck Mexime wa Kagera Sugar ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Novemba Mgunda ametuwezesha kushinda mechi nne dhidi ya Ihefu, Namungo, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania na tukitoka sare dhidi ya Mbeya City na Singida Big Stars.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mgunda kushindika tuzo ya kocha bora wa mwezi tangu ajiunge na kikosi chetu Septemba mwaka huu.

Mgunda amekabidhiwa tuzo hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto huku akipokea mfano wa hundi ya Sh. 1,000,000.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER