Mazoezi ya mwisho Ali Hassan Mwinyi

Kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri tayari kupigania pointi tatu.

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada kubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi kwenye mchezo wa kesho.

Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunaiheshimu Tabora lakini tumejipanga kuhakikisha tunaondoka na alama zote tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER