Matola: Tupo tayari kwa Azam FC Kesho

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza saa 10 jioni.

Matola amesema kikosi kimewasili salama jana usiku kutoka Tabora na wachezaji wapo kwenye hali nzuri kwa ajili ya kuipigania timu.

Matola ameongeza kuwa utakuwa mchezo mgumu kwakuwa ni ‘Derby’ na unahusisha timu ambazo zinapigania ubingwa lakini hata hivyo tumejipanga kuwakabili.

“Mara zote tunapokutana na Azam haiwezi kuwa mechi nyepesi, Azam ni timu kubwa na ina kikosi bora kwahiyo tunategemea kupata upinzani mkubwa ingawa tumejipanga kushinda,” amesema Matola.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wao kama wachezaji wapo kamili na kila atayepata nafasi ya kucheza atakuwa tayari kuipigania timu.

“Morali za wachezaji zipo juu, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Azam lakini tupo tayari kupambana na mwisho wa siku tupate pointi tatu,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER