Kocha Mkuu Pablo Franco, leo atawaanzisha viungo watatu wakabaji katika mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigiwa saa nne usiku kwa saa za nyumbani.
Henock Inonga amepangwa kiungo wa ulinzi sambamba na Erasto Nyoni pamoja na Sadio Kanoute huku Joash Onyango na Kennedy Juma wakisimama kama walinzi wa kati
Nahodha John Bocco ataongoza mashambulizi wakati Peter Banda na Pape Ousmane Sakho wakishambulia kutoka pembeni.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), Henock Inonga (29), Peter Banda (11), Erasto Nyoni (18), John Bocco (22), Sadio Kanoute (13), Pape Sakho (17)
Wachezaji wa akiba
Beno Kakolanya (30), Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Bernard Morrison (3), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu (27) Jimmyson Mwinuke (21).
One Response