Kikosi chetu leo saa tatu usiku kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha Abdelhak Benchikha amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi ya mwisho wa ligi dhidi ya Mashujaa FC uliopigwa Machi 15.
Benchikha amemuanzisha Sadio Kanoute akichukua nafasi ya Freddy Michael Kouablan ambaye yupo benchi.
Hiki hapa kikosi kamili kilivyopangwa:
Ayoub Lakred (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Che Malone (20), Henock Inonga (29), Babacar Sarr (33), Said Ntibazonkiza (10), Fabrice Ngoma (6), Kibu Denis (38), Sadio Kanoute (8), Clatous Chama (17).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), David Kameta (3), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Willy Onana (7), Luis Miqussone (11), Mzamiru Yassin (19), Freddy Michael (18), Pa Omar Jobe (2).