Kagere kuongoza mashambulizi dhidi ya Al Ahly, Nyoni kuanza

Mshambuliaji kinara Medie Kagere ataongoza mashambulizi kwenye mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Al Ahly huku Erasto Nyoni akianza kwenye safu ya kiungo.

Kagere anachukua nafasi ya Chris Mugalu anayeanzia benchi wakati Nyoni amepangwa kwenye nafasi ya Taddeo Lwanga akisaidiana na Jonas Mkude.

Kocha Didier Gomez pia amewaanzisha viungo washambuliaji Clatous Chama, Luis Miquissone na Rally Bwalya ili kuhakikisha tunatengeneza nafasi nyingi na kuzitumia kupata ushindi.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

1. Aishi Manula

2. Shomari Kapombe

3. Mohamed Hussein ©

4. Joash Onyango

5. Pascal Wawa

6. Erasto Nyoni

7. Clatous Chama

8. Jonas Mkude

9. Medie Kagere

10. Rally Bwalya

11. Luis Miquissone

Wachezaji wa Akiba

Gk. Beno Kakolanya

02. Kennedy Juma

03. Mzamiru Yassin

04. Hassan Dilunga

05. Bernard Morrison

06. Chris Mugalu

07. Francis Kahata

2 Comments

  • Posted April 9, 2021 9:28 pm 0Likes
    by Salehe Tulukenzile

    Ninawaombea sana wana msimbazi .. lazima tushinde ameeee .huku azam kashinda vpl ….

  • Posted April 9, 2021 10:19 pm 0Likes
    by eyad

    ماتش الاهلي سيمبا مباشر

Leave a comment