Kagere, Kibu kuongoza mashambulizi dhidi ya KMC

Medie Kagere na Kibu Denis wamepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigwa leo katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi saa 10 jioni.

Kocha Pablo Franco amekuwa akiamini kuwatumia washambuliaji hao kwa kuwa wamekuwa na uelewano mzuri uwanjani.

Kagere na Kibu watapata huduma ya karibu kutoka kwa viungo washambuliaji, Pape Sakho na Rally Bwalya ambao watatokea pembeni.

Jonas Mkude na Mzamiru Yassin wamepangwa katika kiungo wa ulinzi huku Joash Onyango na Henock Inonga wakicheza pamoja kama mabeki wakati.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (17), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38), Rally Bwalya (8)

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Gadiel Michael (2), Pascal Wawa (6), Abdulsamad Kassim (25), Hassan Dilunga (24), Ibrahim Ajibu (10), Chris Mugalu (7), Yusuf Mhilu (27), Jimmyson Mwinuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER