Hiki hapa kikosi cha Gomez dhidi ya Kagera

Kocha Mkuu, Didier Gomez na wasaidizi wake wamepanga kikosi kamili kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya 16 bora dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa leo saa moja usiku.

Gomez amewaanzisha mlinda mlango namba moja Aishi Manula akisaidiwa na walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango na Pascal Wawa.

Katika eneo la kiungo wa ukabaji amewaanzisha Taddeo Lwanga na Jonas Mkude huku washambuliaju wakiwa ni Clatous Chama, Luis Miquissone na Rally Bwalya wakati idara ya ushambuliaji itaongozwa na Medie Kagere.

Baadhi ya wachezaji wanaoanzia benchi ni washambuliaji John Bocco, Chris Mugalu na kiungo mshambuliaji Bernard Morrison.

Kikosi Kamili kilichopangwa

1. Aishi Manula

2. Shomari Kapombe

3. Mohamed Hussein ©

4. Joash Onyango

5. Pascal Wawa

6. Taddeo Lwanga

7. Clatous Chama

8. Jonas Mkude

9. Medie Kagere

10. Rally Bwalya

11. Luis Miquissone

Wachezaji wa Akiba

Gk. Beno Kakolanya

02. David Kameta

03. Erasto Nyoni

04. Mzamiru Yassin

05. Chris Mugalu

06. John Bocco

07. Bernard Morrison

SHARE :
Facebook
Twitter

6 Responses

  1. Tunawaombea uzima usiokua na malazi pia tunawapa pongezi benchi la ufundi pamoja na wachezaje na viongozi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER