Chama azidi kung’ara Ligi ya Mabingwa Afrika

Kiungo mshambuliaji, Clatous Chama amechaguliwa mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa Afrika mzunguko wa tano kutokana na kiwango bora alichokionyesha katika mchezo wetu dhidi ya AS Vita uliopigwa Aprili 3, mwaka huu.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Chama alifunga mabao wawili na kusaidia kupatikana kwa ushindi wa 4-1.

Chama raia wa Zambia amewashinda Amiri Sayoud (CR Belouizdad) Ricardo Goss (Mamelod Sundowns) na Ferjan Sassi (Zamalek) kwa kupata asilimia 51 ya kura zilizopigwa.

Chama anakuwa mchezaji wa pili kutoka kwenye kikosi chetu kuchaguliwa mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa baada ya Luis Miquissone kufanya hivyo mwezi uliopita.

2 Comments

  • Posted April 8, 2021 7:33 pm 0Likes
    by Anania sabaya

    Naipenda sana simba hakika kombe la club bingwa litatua msimbazi

  • Posted April 8, 2021 10:08 pm 0Likes
    by Johnson jr

    Kesho linakufa jitu 3-0

Leave a comment