Bocco, Ntibazonkiza wapiga hat trick tukiichakaza Prisons ‘wiki’

 

Nahodha John Bocco na kiungo Said Ntibazonkiza wamefunga magoli matatu (hat trick) kila mmoja katika ushindi mnono wa mabao 7-1 tuliopata dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Nahodha John Bocco alitupatia bao la kwanza dakika ya 14 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Said Ntibazonkiza.

Mlinzi wa kati Henock Inonga alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 24 baada ya kuumizwa na Samson Mbangula ambaye alionyeshwa kadi nyekundu.

Prisons ilisawazisha bao hilo dakika ya 30 kupitia kwa Jeremiah Juma kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Salum Kimenya kuokolewa na Aishi Manula kabla ya kumkuta mfungaji.

Dakika ya 47 Bocco alitupatia bao la pili baada ya kupokea mpira wa krosi uliopigwa na Pape Sakho ambaye alimzidi ujanja mlinzi wa Prisons kabla ya kutoa pasi.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la tatu dakika ya 60 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Clatous Chama na kupiga shuti kali la chini chini akiwa ndani ya 18.

Bocco alikamilisha hat trick kwa kufunga bao la nne 63 kwa kichwa kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Clatous Chama kuokolewa na mlinda mlango Hussein Abel kabla ya kumkuta.

Dakika moja baadaye, Ntibazonkiza alitupatia bao la tano baada ya kupokea pasi kutoka kwa kiungo mkabaji Mzamiru Yassin.

Ntibazonkiza naye alikamilisha hat trick yake dakika ya 70 baada ya kufunga bao la sita akipokea pasi kutoka kwa Chama.

Mlinzi Shomari Kapombe alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la saba dakika ya 88 kwa kichwa kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Gadiel Michael.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Henock, Bocco, Sakho, Mohamed Hussein na Sadio Kanoute na kuwaingiza Kennedy Juma, Augustine Okrah, Habib Kyombo, Victor Akpan na Gadiel.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER