Mshambuliaji Jentrix Shikangwa amekabidhiwa tuzo yake ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) 2022/23.
Shikangwa amekabidhiwa kiatu cha dhahabu katika hafla ya tuzo za TFF 2022/23 zinazofanyika jijini Tanga usiku huu.
Shikangwa pia amechaguliwa katika kikosi bora cha SLWPL msimu wa 2022/23.
Wachezaji wengine walioingia kwenye kikosi bora cha msimu ni pamoja na walinzi Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ na Violeth Nicholas.