Wachezaji tisa kutoka kwenye kikosi chetu wameitwa katika Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayojiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Uganda.
Baada ya kuonyesha kiwango safi katika mechi za maandalizi ya msimu (Pre Season) mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya naye amejuimuishwa kikosini.
Kiungo mkabaji Jonas Mkude na mshambuliaji mpya Habib Kyombo nao ni miongoni mwa nyota 25 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwa ajili ya mechi hizo.
Wachezaji hao walioitwa ni walinda mlango
Aishi Manula
Beno Kakolanya
walinzi
Shomari Kapombe
Mohamed Hussein
Kennedy Juma
Viungo
Jonas Mkude
Mzamiru Yassin
Washambuliaji
Kibu Denis
Habib Kyombo
Stars itaingia kambini Jumapili na mchezo wa kwanza utapigwa Agosti 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa na marudio itakuwa Septemba 3 jijini Kampala, Uganda.