Timu yafanya mazoezi ya mwisho Liti

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho jioni kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Uwanja wa Liti saa 10 jioni.

Mazoezi hayo ambayo yamesimamiwa na Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake yamefanyika katika Uwanja wa Sokoine ambao tutautumia kesho kwenye mchezo.

Wachezaji wote 22 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi ya kucheza kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER