Zimbwe Jr ataja sababu ugumu wa mechi dhidi ya Gwambina

Mfungaji wa bao pekee katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Gwambina FC, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema mazingira ya Uwanja wa Gwambina hayakuwa rafiki jambo lililosababisha mechi kuwa ngumu.

Zimbwe amesema iliwalazimu wachezaji kucheza soka la mipira mirefu ya juu sababu uwanja haukuruhusu soka letu la kawaida la pasi fupi fupi tulilolizoea.

Mlinzi huyo wa kushoto amesema amefurahi kufunga bao la ushindi ambalo limetuwezesha kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu huu ulipoanza.

“Tulisubiri kwa muda mrefu siku hii kufika na tulipambana hadi kufanikisha kukaa kileleni, binafsi nimefurahi kufunga bao la ushindi ambalo limetupandisha hadi nafasi ya kwanza,” amesema Zimbwe.

Zimbwe ameongeza kuwa malengo ya timu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ili kutetea ubingwa ambapo kama tutafanikiwa itakuwa ni mara ya nne mfululizo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER