Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally, amemtangaza nguli wa Bongo Fleva, Ally Kiba kuwa mtumbuizaji mkuu kwenye Tamasha la Simba Day litakalofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 3.
King Kiba atatoa burudani kwa mara ya pili mfululizo kwenye Tamasha la Simba Day akiwa mtumbuizaji kinara baada ya kufanya hivyo mwaka jana.
Ahmed amesema King Kiba ni Mwanamuziki mwenye uwezo mkubwa na anayeoendwa na Wanasimba ndio maana atatumbuiza siku hiyo.
Ahmed ameongeza kuwa mbali na King Kiba Burudani zitakuwa nyingi na wasanii mbalimbali watakaotumbuiza wataendelea kutangazwa kuanzia leo hadi siku ya kilele.
“Kama kawaida fundi wa Bongo Fleva Ally Kiba atatumbuiza kwenye kilele cha Simba Day. King Kiba hana haja ya kumuelezea sana, anajielezea mwenyewe,” amesema Ahmed.
Akizungumzia Simba Day yenyewe Ahmed amesema “mwaka huu itakuwa ya tofauti hivyo Wanasimba wahakikishe wananunua tiketi mapema.”