Zimbwe Jr aelezea Maandalizi ya mchezo dhidi ya Singida Big Stars

Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa Ijumaa Uwanja wa Benjamin Mkapa yanaendelea vizuri.

Zimbwe Jr amesema kila mchezaji anafahamu ugumu wa mchezo na ratiba ngumu tuliyonayo katika mwezi huu kwahiyo kila mchezo kwetu ni fainali.

“Sisi kama wachezaji tunafahamu tuna ratiba ngumu katika mwezi huu, tunataka kuhakikisha tunautumia mchezo dhidi ya Singida kupata ushindi na kuongeza morali ndani ya kikosi.

“Mchezo wa kwanza dhidi ya Singida uliisha kwa sare, kuna mapungufu yaliyojitokeza ambayo tunayafanyia kazi mazoezini na mazuri tutayaendeleza kitu kizuri mwalimu amerudi.

“Kikubwa tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi, tunawahitaji sana kipindi hiki kwa ajili ya kuongeza hamasa,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER