Watano waitwa Taifa Stars

Wachezaji wetu watano wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinachojiandaa na michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Stars itacheza mechi mbili za kufuzu CHAN dhidi ya Somalia ambapo wachezaji wanakiwa kuwasili kambini keshokutwa Ijumaa.

Wachezaji hao ni mlinda mlango Aishi Manula walinzi Mohamed Hussein na Kennedy Juma kiungo Mzamiru Yassin na mshambuliaji Kibu Denis.

Nyota hao hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakacho ondoka kesho nchini kuelekea Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu ambapo wataungana na wenzao mara tu wakimaliza majukumu ya timu ya Taifa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER