Uongozi wa klabu umetaja viingilio vya mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold utakaopigwa kesho saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Viingilio hivyo vitakuwa kwenye Jukwaa la Mzunguko Sh 5,000
VIP B na C Sh 10,000
VIP A Sh 15,000
Mchezo wa kesho tutautumia kama sehemu ya maandalizi ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows itakayopigwa Desemba 5, nchini Zambia.
Mashabiki wetu wanaombwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu ili kuongeza hamasa na tubaki na alama tatu katika uwanja wa nyumbani.
2 Responses
Simba nguvu moja.