Kaimu Kocha Mkuu Seleman Matola, amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wetu wa mwisho wa kufungia msimu dhidi ya Mbeya Kwanza utakaopigwa kesho saa 10 jioni Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Matola amesema hali ya hewa ni baridi lakini haitakuwa changamoto kwa kuwa tulianza kufika jijini Mbeya ambapo hakuna tofauti kubwa.
Matola amesema hautakuwa mchezo rahisi na anategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mbeya Kwanza lakini tumejipanga kuhakikisha tunaondoka na pointi zote tatu.
“Maandalizi yamekamilika, leo asubuhi tumefanya mazoezi ya mwisho na wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho.
“Mchezo utakuwa mgumu najua Mbeya Kwanza watataka kupata ushindi hata kama wameshuka lakini sisi tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Matola.