Tupo tayari kupigania pointi tatu dhidi ya Namungo leo

Kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya kupambania alama tatu muhimu kutoka kwa Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Katika mchezo huo tunahitaji kupata alama tatu ili kurejesha imani kwa mashabiki pamoja na hali ya kujiamini kwa wachezaji wetu.

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema kwa sasa tunapitia kipindi kigumu wachezaji wanacheza kwa presha kubwa lakini benchi la ufundi linashughulikia kuwarejesha katika hali zao.

Matola amesema morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kupambana kuhakikisha tunawapa furaha Wanasimba leo.

“Tunapitia kipindi kigumu, wachezaji wanacheza kwa presha ndiyo maana tunapoteza nafasi nyingi lakini tunaendelea kulifanyia kazi na kuelekea mechi ya leo kutakuwa na mabadiliko makubwa,” amesema Matola.

NYOTA SITA KUIKOSA NAMUNGO LEO

Kuelekea mchezo wa leo tutakosa huduma ya wachezaji wetu watano ambao ni majeruhi huku mmoja akitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Wachezaji ambao ni majeruhi ni Chris Mugalu, Pape Ousmane Sakho, Taddeo Lwanga, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin.

Mlinzi wa kati Henock Inonga Baka nae atakosekana kwenye mchezo wa leo na mechi nyingine mbili zijazo za ligi kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER