Tupo Sokoine leo kuikabili Mbeya City

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Sokoine saa 10 jioni kuikabili Mbeya City katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tunaingia katika mchezo wa leo tukiwa tunajua tunakutana na timu imara yenye wachezaji bora lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi.

Wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Itende jana na wapo kwenye hali nzuri tayari kupambana kupata alama tatu muhimu kwenye mchezo wa leo.

MGUNDA: TUPO TAYARI KWA MCHEZO

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali tayari kwa mchezo wa leo na maandalizi yamekamilika.

Mgunda amesema tunaiheshimu City na tunategemea kupata ushindani mkubwa hasa katika Uwanja wa Sokoine lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

“Tunaiheshimu Mbeya City, ni timu nzuri na imejipanga vizuri lakini nasi tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani na tupo tayari kwa mpambano.

HALI YA KIKOSI

Wachezaji wote 22 waliosafiri ambao wote wamefanya mazoezi jana na wapo tayari kwa mchezo wa leo.

Tutaendelea kukosa huduma ya Israel Patrick na Jimmyson Mwanuke ambao wanaendelea na mazoezi mepesi huku Peter Banda na Nelson Okwa wakiendelea na matibabu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER