Tupo kwa Mkapa kuikabili Namungo leo

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku kuikabili Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tupo kwa Mkapa kuikabili Namungo leo

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku kuikabili Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tunaingia katika mchezo wa leo tukiwa tunajua tunakutana na timu imara yenye wachezaji bora pamoja na benchi bora la ufundi lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi.

Wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena na wapo kwenye hali nzuri tayari kupambana kupata alama tatu muhimu kwenye mchezo wa leo.

MGUNDA ASISITIZA LIGI NI NGUMU

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesisitiza kuwa ligi ni ngumu na kila timu imejipanga kupata alama tatu katika uwanja wowote iwe nyumbani au ugenini.

Mgunda amesema ligi inavyozidi kusonga ugumu unazidi kuongezeka na kila timu tunayokutana nayo inakuwa imejipanga kutafuta alama tatu.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, wachezaji wapo kwenye hali nzuri kwa ajili ya mechi ambayo tunaamini itakuwa ngumu. Kadiri ligi inavyosonga mbele ndiyo inavyozidi kuwa ngumu,” amesema Mgunda.

ALLY SALIM AWAITA MASHABIKI KWA MKAPA

Mlinda mlango Ally Salim, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kutupa sapoti kwakuwa wana mchango mkubwa wa hamasa hasa kipindi hiki ugumu wa ligi ukiwa umeongezeka.

“Mashabiki ni watu muhimu tunawahitaji kwenye mchezo wa leo, tunajua utakuwa mgumu. Namungo ni timu bora lakini tupo tayari kupambana kupata pointi tatu nyumbani,” amesema Salim.

MWANUKE, MWENDA WAANZA MAZOEZI

Winga Jimmyson Mwanuke na mlinzi wa kulia Israel Patrick ambao walikuwa majeruhi wameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari na wanatarajia kurudi uwanjani siku chache zijazo.

MKUDE, OKWA BADO

Viungo Jonas Mkude na Nelson Okwa bado hali zao hazijatengemaa hivyo hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER