Tunaanza safari yetu ya NBCPL 2023/24

Alhamisi ya Agosti 17 saa 10 jioni katika Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro kikosi chetu kitatupa karata ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC msimu ya 2023/24 kwa kuwakabili ‘Wakata Miwa’ Mtibwa Sugar.

Alhamisi itakuwa tunaanza rasmi safari ya kurejesha mataji yote yaliyopotea miaka miwili iliyopita.

Jumapili Agosti 14 katika Uwanja wa CCM Mkwakwani tumechukua Ngao ya Jamii kwa kuwafunga watani Yanga kwa mikwaju ya penati 3-1.

Baada ya kupata taji la kwanza Jumapili sasa nguvu yetu tunaielekeza kwenye Ligi kuhakikisha tunapata alama kwenye kila mchezo tukianza Alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Robertinho: Tunautaka Ubingwa wa NBCPL 2023/24

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi dhamira ya kila Mwanasimba ni kuhakikisha ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 unakuwa wetu.

Robertinho amesema yeye na benchi lake zima la ufundi pamoja na wachezaji wapo tayari kuhakikisha tunapambana kufikia malengo tuliyojiwekea.

“Msimu huu tumedhamiria kuwa mabingwa Ligi Kuu ya NBC, karata yetu ya kwanza ipo Morogoro dhidi ya timu ngumu ya Mtibwa Sugar.

“Wachezaji wana ari kubwa na wanaamini wana kila sababu ya kuwa mabingwa na wapo tayari kupambana katika kila dakika 90 msimu huu ili tufanikishe malengo yetu,” amesema Robertinho.

NBCPL Kupigwa ndani ya Mikoa 11……

Msimu wa Ligi Kuu ya NBC unaanza leo Agosti 15 na kuhitimika Mei 29 mwakani na utashirikisha timu 16 kutoka Mikoa 11 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mikoa hiyo ni kama ifuatavyo na timu zake kwenye mabano.

Dar es Salaam (Simba SC, Yanga SC, Azam FC, KMC, JKT Tanzania).

Mbeya (Tanzania Prisons, Ihefu FC)

Dodoma (Dodoma Jiji FC)

Tanga (Coastal Union)

Kagera (Kagera Sugar)

Singida (Singida Fountain Gate FC)

Kigoma (Mashujaa FC)

Lindi (Namungo FC)

Geita (Geita Gold FC)

Tabora (Kitayosce FC)

Morogoro (Mtibwa Sugar)

Tunafahamu kuwa ili tuwe mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 tunapaswa kukusanya alama nyingi zaidi ya timu zote 15 hapo juu.

Tunafahamu haitakuwa kazi rahisi lakini tumejipanga na tupo tayari kupambana kupigania malengo tuliyojiwekea.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER