Tumetinga Robo fainali Mabingwa Afrika kibabe

Tumefanikiwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kibabe baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza dakika ya sita baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na Clatous Chama.

Pa Omar Jobe aliongeza bao la pili dakika ya 12 baada kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Kibu Denis alitupatia bao la tatu dakika ya 22 akimalizalia pasi ya Chama ambaye alimlamba chenga mlinzi wa Jwaneng kabla ya kutoa pasi.

Chama alitupatia bao la nne dakika ya 76 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ntibazonkiza na kupiga shuti kali akiwa ndani ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa Jwaneng.

Ladaki Chasambi alitupatia bao la tano dakika ya 87 baada ya krosi iliyopigwa na Freddy Michael kuokolewa na mlinda mlango wa Jwaneng kabla ya kumkuta mfungaji.

Fabrice Ngoma alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la sita dakika ya 90 kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein.

Matokeo haya yametufanya kufikisha pointi tisa tukiwa nafasi ya pili kwenye kundi alama moja nyuma ya vinara ASEC Mimosas.

X1: Ayoub, Shomari, Zimbwe Jr, Che Malone, Henock Ngoma (Hamis 92+3′), Kibu (Chasambi 82:), Babacar (Mzamiru 61′) Jobe (Freddy 82′), Ntibazonkiza (Miqussone 82′), Chama

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER