Tumeshusha Chuma kutoka Serbia

Klabu yetu imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Dejan Georgijević (28), raia wa Serbia kwa mkataba wa miaka miwili.

Msimu uliopita Dajan alikuwa anacheza katika timu ya NK Domzale ya Slovenia ambayo ilishiriki michuano ya Uefa Conference League.

Mbali na timu hiyo Dajan amewahi kuzitumikia timu mbalimbali kama FK Partizan FC Irtysh Pavlodar, Ferencvárosi TC, FK Voždovac.

Dajan anakuja kuongeza nguvu katika idara yetu ya ushambuliaji ambapo anaungana nyota wengine kama Nahodha John Bocco, Moses Phiri na Habib Kyombo.

Usajili wa Dajan unakuwa wa nane msimu huu baada ya Nelson Okwa Moses Phiri, Augustine Okrah, Victor Akpan, Habib Kyombo, Nassor Kapama na Mohamed Ouattara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER