Tumepoteza nyumbani dhidi ya Al Ahly

Mchezo wetu wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.

Al Ahly walipata bao mapema dakika ya nne kupitia kwa Ahmed Kouka baada ya mpira wa krosi uliopigwa Mohamed Hany kushindwa kuzuiliwa vizuri na mlinzi Henock Inonga kabla ya kumkuta mfungaji.

Baada ya bao hilo Al Ahly walirudi nyuma wakizuia na kutuacha tumiliki mpira huku wao wakifanya mashambulizi machache ya kushtukiza.

Hata hivyo tulistahili kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa zaidi ya mabao mawili baada ya kupoteza nafasi mbili za wazi kupitia kwa Sadio Kanoute na Saido Ntibazonkiza.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuendelea kuliandama lango la Al Ahly lakini tulikosa umakini wa kutumia nafasi tulizotengeza.

Mchezo wa marudiano utapigwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo nchini Misri Aprili 5 na mshindi wa jumla atasonga mbele na kutinga nusu fainali.

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Inonga, Babacar (Mzamiru 79′), Ntibazonkiza (Jobe 79′) Ngoma, Kibu, Kanoute (Onana 45′), Chama

Walioonyeshwa kadi: Babacar 49′ Inonga 56′

X1: Shobeir, Abd ElMonem, Rabia, Hany, Maaloul, Marawan (Afsha 70′), Koka, El Soulia, El Shahat (Reda Slim 67′) , Tau (Taher 67′), Modeste (Kahraba 70′)

Walioonyeshwa kadi: Marwan Attia 53′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER