Tumepoteza Mchezo wa Fainali

Mchezo wetu wa fainali ya Kombe la Mapinduzi umemalizika na tumepoteza kwa kufungwa bao moja na Mlandege FC katika mtanange uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukimiliki sehemu kubwa na kutengeneza nafasi lakini Mlandege walikuwa makini katika idara ya ulinzi.

Joseph Akandanao aliwatanguliza Mlandege kwa kuwapa bao la kwanza dakika ya 54 baada ya kuwapiga chenga walinzi watatu kabla ya kupiga shuti la chini chini liliomshinda mlinda mlango Ayoub Lakred.

Baada ya bao hilo Mlandege walirudi nyuma wote huku tukishambulia zaidi lakini hata hivyo bahati haikuwa yetu.

Mlandege wameweka historia ya kuchukua taji la michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo.

X1: Lakred, Kapombe, Israel, Kazi, Che Malone, Babacar (Hamis 59′), Miqussone (Ladack 78′), Ngoma, Phiri (Baleke 45′), Ntibazonkiza, Onana (Karabaka 83′)

Walioonyeshwa kadi:

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER