Tumepoteza mchezo dhidi ya Haras El Hodoud

Mchezo wetu wa kirafiki uliopigwa katika mji wa Cairo umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Haras El Hodoud ambao wamepanda daraja kucheza ligi kuu nchini Misri msimu ujao.

Haras walianza mpira kwa kasi ambapo walifanikiwa kupata bao la mapema dakika ya pili kwa mkwaju wa penati lililofungwa na Mahmoud Guda.

Mshambuliaji Moses Phiri alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 41 baada ya kupata maumivu nafasi yake ikachukuliwa na Victor Akpan.

Iliwachukua dakika 10 baada ya Kipindi cha pili Haras kuongeza bao la pili lililofungwa na Mahmoud Mamduh baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu.

Winga Peter Banda almanusura atupatie bao dakika ya 59 lakini mlinda mlango wao alifanya kazi kubwa ya kuokoa.

Kocha Zoran Maki alifanya mabadiliko ya kuwatoa Gadiel Michael, Clatous Chama na Augustine Okrah na kuwaingiza Nassoro Kapama, Erasto Nyoni na Habib Kyombo.

Aidha, Kocha Zoran aliwatoa Joash Onyango na Jonas Mkude na kuwaingiza Taddeo Lwanga na Jimmyson Mwanuke.

Mchezo huu ni wa tatu wa kujipima nguvu hapa nchini Misri ambapo kocha Zoran anaendelea kukiandaa kikosi chetu tayari kwa kuanza msimu mpya wa ligi 2022/23.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER