Tumepoteza mbele ya Arta Solar 7

Mchezo wetu wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Arta Solar 7 kutoka Djibouti uliopigwa Uwanja wa Uhuru umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kadiri huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini hakuna aliyeweza kutumia nafasi ilizopata kipindi cha kwanza.

Mlinda mlango wa Arta, Chris Dilo alikuwa nyota wa mchezo baada ya kuokoa michomo miwili ya Peter Banda kipindi cha kwanza na Dejan Georgijevic cha pili.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kuendelea kuliandama pango la Arta lakini hata hivyo mlinda mlango Dilo aliendelea kubaki kikwazo.

Athumani Manucho aliwapatia bao hilo pekee Arta dakika ya 89 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu.

Kocha Zoran Maki aliwaingiza Dejan, Aboubakar Hamis na Omary Mfaume kuchukua nafasi za Moses Phiri, Sadio Kanoute na Israel Mwenda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER