Tumepoteza mbele ya Al Dhafrah

Mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Al Dhafrah uliofanyika katika Mji wa Abu Dhabi umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.

Mchezo ulikuwa mzuri ambapo tulimiliki sehemu kubwa hasa kipindi cha kwanza lakini tulishindwa kuzitumia nafasi tulizotengeneza.

Kipindi cha pili tuliendelea kucheza vizuri tukifanya mashambulizi huku wenzetu wakifanya machache na kufanikiwa kupata bao dakika ya 78.

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ alifanya mabadiliko ya kuwatoa Kennedy Juma, Jonas Mkude na Pape Sakho na kuwaingiza Mohamed Ouattara, Erasto Nyoni na Kibu Denis.

Baada ya mchezo kikosi kinarejea Dubai kujiandaa na mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow utakaopigwa Jumapili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER