Mchezo wetu watatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika tuliocheza na Wydad Casablanca katika Uwanja wa Marrakech nchini Morocco umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja.
Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini mechi ikichezwa zaidi katikati ya uwanja.
Mlinda mlango, Ayoub Lakred alicheza mkwaju wa penati uliopigwa na nahodha, Yahya Jabrane dakika ya 41 baada ya Kibu Denis kumchezea madhambi Saifdine Bouhra ndani ya 18.
Kipindi cha pili tuliendelea kushambuliana kwa zamu lakini ufanisi wa kutumia nafasi zilizopatikana ulikuwa mdogo.
Zakaria Draoui aliwapatia wenyeji bao la ushindi dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jabrane.
X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Henock, Che Malone, Ngoma, Kibu (Phiri 75′), Kanoute (Mzamiru 75′), Baleke, Ntibazonkiza (Miqussone 90′), Onana (Chama 58′)
Walioonyeshwa kadi: Ntibazonkiza 46′ Kanoute 48′ Lakred 88′ Baleke 90+1