Tumepoteza Derby ya Kariakoo

Mchezo wetu wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Yanga uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 5-1.

Yanga walipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa Kennedy Musonda kwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Yao Attohoula.

Kibu Denis alitupatia bao la kusawazisha kwa kichwa dakika ya tisa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Said Ntibazonkiza.

Max Nzengeli aliwapatia Yanga bao la pili dakika ya 64 kwa shuti kali la chini chini baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu wa Kati.

Aziz Ki aliwapatia Yanga bao la tatu dakika ya 72 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clement Mzize.

Nzengeli aliwapatia Yanga bao la nne dakika ya 77 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi ya Mzize.

X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Henock, Ngoma, Kibu (Miquissone 59′), Kanoute (Mzamiru 76′), Baleke (Phiri 71′), Ntibazonkiza, Chama (Onana 76′)

Walioonyeshwa kadi: Ngoma 23′ Chama 56′ Che Malone 85′

X1: Diara, Yao, Lomalisa (Kibabage 88′), Job, Baka (Mwamnyeto 88′), Aucho, Nzengeli (Skudu 88′) Mudathir (Mkude 83′) Musonda (Mzize 72′), Aziz Ki, Pacome

Walioonyeshwa kadi: Job 7′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER