Tumepata ushindi mnono dhidi ya Cosmo

Kikosi chetu kimepata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Cosmopolitan katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Mo Simba, Bunju.

Moses Phiri alitupatia bao la kuongoza kwa mtindo wa tikitaka dakika ya 14 baada ya mpira wa krosi kuokolewa vibaya na mabeki wa Cosmopolitan kabla ya kumkuta.

Jean Baleke alitupatia bao la pili dakika ya 16 baada ya mabeki wa Cosmopolitan kushindwa kuhokoa pasi iliyopigwa na Phiri.

Dakika ya 25, Willy Onana alitupatia bao la tatu baada ya krosi ya Mohamed Hussein kupigwa kichwa na Shomari Kapombe na kumtengea mfungaji.

Cosmopolitan walipata bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 36 kufuatia Kapombe kuokoa mpira uliokuwa unaelekea wavuni kwa mkono kosa ambalo lilipelekea kuonyeshwa kadi nyekundu.

Dakika ya 57 kocha Roberto Oliviera ‘Robertinho’ alifanya mabadiliko ya kuiwangiza Jimmyson Mwanuke, Aubin Kramo, Abdallah Khamis na Nassor Kapama na kuwatoa Fabrice Ngoma, Zimbwe Jr, Phiri na Sadio Kanoute.

Dakika ya 58, Kramo alitupatia bao na nne kwenye mpira wake wa kwanza kugusa baada ya mpira mfupi wa kona uliyopigwa na Luis Miquissone kumkuta na kuunganisha moja kwa moja.

Robertinho alifanya mabadiliko mengine ya kuwatoa Onana, Baleke na Ayoub Lakred na kuwaingiza Shaban Chilunda, Mohamed Mussa na Hussein Abel.

Dakika 85 Chilunda alikamilisha karamu ya mabao kwa kufinga bao zuri la tano baada ya kupiga shuti kali nje ya 18.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER