Tumepata ushindi dhidi ya Dar City

Kikosi chetu kimepata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dar City katika mchezo wa kirafiki iliyofanyika Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju.

Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mlinzi wa kati Che Fondoh Malone alitupatia bao la kwanza dakika ya 40 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mohamed Hussein Zimbwe Jr.

Dakika mbili baadaae kiungo mshambuliaji, Willy Onana alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati baaada ya Shaban Chilunda kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Baaada ya mabao hayo tuliendelea kulisakama lango la Dar City lakini mpaka tunaenda mapumziko tulikuwa mbele kwa mabao hayo.

Israel Patrick alitupatia bao la tatu kabla ya Moses Phiri kukamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne dakika ya 75 baada ya kupokea pasi ya kisigino kutoka kwa nahodha John Bocco.

Katika mchezo huo kocha Daniel Cadena alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mzamiru Yassin, Onana, Che Malone na Ayoub Lakred na kuwaingiza Abdallah Khamis, David Kameta, Nassor Kapama na Ally Salim.

Kikosi kilichoanza

Ayoub Lakred (40)
Israel Patrick (5)
Mohamed Hussein (15)
Hussein Kazi (16)
Kennedy Juma (26)
Che malone (20)
Fabrice Ngoma (6)
Mzamiru Yassin (19)
Shaban Chilunda (27)
Moses Phiri (25)
Willy Onana (7)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER