Tumepata tuzo ya mashabiki bora AFL

Mashindano ya African Football League (AFL) yamemalizika leo huku Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikitawazwa mabingwa kwa kuifunga Wydad Casablanca ya Morocco mabao 2-0.

Michuano hiyo imeshirikisha timu nane za Afrika huku Simba ikiwa ndio pekee kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati iliyopata nafasi ya kushiriki.

Baada ya kuhitimishwa michuano hiyo ambayo ndio mara ya kwanza kufanyika barani Afrika Simba tumefanikiwa kutwaa tuzo ya mashabiki bora wa mashindano.

Tumepata tuzo hiyo baada ya mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi na kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa katika hafla ya ufunguzi ya michuano hiyo iliyofanyika Oktoba, 20 tulipocheza na Al Ahly kutoka Misri.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameipokea tuzo hiyo baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali kati ya Mamelodi na Wydad.

Baada ya kupokea tuzo hiyo Try Again amesema “Tuzo hii ni kwa kila shabiki wa Simba. Kuja kwenu kuishangilia timu yenu kumeiwezesha timu yetu kushinda tuzo ya mashabiki bora wa AFL. Pongezi nyingi kwenu.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER