Tumepata pointi tatu nyumbani

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Ihefu FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Tulianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Ihefu kutafuta bao la mapema lakini tulikosa njia ya kuifungua safu yao ya ulinzi.

Dakika zote 45 za kipindi cha kwanza Ihefu walicheza kwa kuzuia na kuwa wengi upande wao huku wakiwa hawajafanya shambulizi lolote langoni kwetu.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi tena kukimiliki mpira huku Ihefu nao wakionekana kufunguka na kufanya mashambulizi machache ambayo hata hivyo hayakuwa na madhara.

Pape Sakho alitupatia bao la kwanza dakika ya 63 kwa shuti kali la mguu wa kulia akiwa nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Moses Phiri.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Habib Kyombo, Sakho na Augustine Okrah na kuwaingiza Kibu Denis, Victor Akpan na Nassor Kapama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER