Tumepata alama tatu mbele ya Kagera

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Uwanja wa Uhuru umemalizika kwa kupata ushindi wa mabao 3-0.

Tulianza mchezo kwa kasi huku tukitengeneza nafasi lakini kikwazo kikubwa kikiwa kwa mlinda mlango wa Kagera, Ramadhani Chalamanda.

Said Ntibazonkiza alitupatia bao la kwanza dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na mlinzi wa kati, Denis Bukenya.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kuzidi kufika zaidi langoni mwa Kagera lakini mashambulizi yetu mengi yakiishia kwa Chalamanda.

Sadio Kanoute alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 75 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Nahodha John Bocco alitupatia bao la tatu dakika ya 90 baada ya kutumia makosa yaliyofanywa na mlinzi Abdallah Mfuko kurudisha mpira kwa mlinda mlango kabla ya kuiwahi na kumfunga kirahisi Chalamanda.

Huu ni mchezo wa kwanza wa Ligi kwa kocha Abdelhak Benchikha kukiongoza kikosi chetu huku tukipata ushindi mnono bila kuruhusu bao.

X1: Lakred, Shomari, Zimbwe Jr, Che Malone, Henock, Ngoma, Kanoute, Mzamiru (Kibu 63′), Phiri (Baleke 63′), Ntibazonkiza (Bocco 84′), Chama (Onana 63′)

Walioonyeshwa kadi:

X1: Chalamanda, Mhilu, Disani (Luhende 45′), Bukenya, Mfuko, Shamte, Mashaka (Mkandala 70′), Ally Nassoro (Kiza 75′), Chirwa, Kasozi, Mafie (Anuary 57′)

Walioonyeshwa kadi: Ally Nassoro 25′ Ally Mashaka 81′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER