Tumepangwa na Eagle FC hatua ya pili ASFC

Droo ya hatua ya pili ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) imekamilika na tumepangwa na Eagle FC kutoka Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa droo sisi tutakuwa wa wenyeji wa Eagle na mchezo utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mechi zote za hatua ya pili ambayo itahusisha timu 64 kutoka Ligi Kuu, Championship, Daraja la Kwanza na Mabingwa wa Mikoa zitaanza kupigwa kuanzia Desemba 9-11.

Msimu uliopita tulilipoteza taji hili lakini moja ya malengo yetu msimu huu ni kuhakikisha tunalirejesha mikononi mwetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER