Tumechukua tatu kutoka kwa Kagera

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukiwashambulia zaidi Kagera na kufika zaidi langoni mwao lakini tulipoteza umakini katika eneo la mwisho.

Moses Phiri alitupatia bao la kwanza dakika ya 41 kwa kichwa baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Clatous Chama kugonga mwamba kabla ya kumkuta mfungaji.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi tukiendelea kumiliki na kufanya mashambulizi ambayo mengi yaliishia mikononi mwa Kipao.

Dejan Georgijevic alitupatia bao la pili dakika ya 81 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya mlinda mlango Said Kipao kushindwa kuokoa krosi ya Israel Patrick.

Kocha Zoran Maki aliwatoa Shomari Kapombe, Phiri, Peter Banda, Augustine Okrah na Pape Sakho na kuwaingiza Israel Patrick, Dejan, Mzamiru Yassin, Nelson Okwa na Habib Kyombo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER