Try Again ashiriki kozi ya FIFA Saudi Arabia

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ ameshiriki kozi ya Diploma ya Uongozi wa klabu inayotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ambayo imefanyika Jeddah, Saudi Arabia.

Washiriki wa kozi hiyo ambao ni viongozi wa klabu kutoka sehemu mbalimbali duniani wameshuhudia mchezo wa Kombe la Dunia kwa klabu kati ya Al Ittihad dhidi ya Auckland City ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya kozi hiyo.

Akiwa kwenye kozi hiyo Try Again amekutana na viongozi mbalimbali wa soka duniani kama Rais wa FIFA, Gianni Infantino, Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura na wengineo.

Akizungumzia akiwa kwenye kozi hiyo, Try Again amesema “nipo Saudi Arabia nashiriki kozi ya Uongozi wa klabu inayotolewa na FIFA kwa viongozi wa klabu mbalimbali duniani.

“Nimepata bahati ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi kutoka klabu kubwa duniani kama Manchester United na Liverpool lengo likiwa ni kubadilisha uzoefu katika jinsi ya kuziongoza klabu,” amesema Try Again.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER