Timu yawasili salama Dar

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam kutoka Ndola; Zambia baada ya kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos uliopigwa Jumamosi iliyopita.

Baada ya kikosi kurejea kimeingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Alhamisi.

Jana kikosi kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili kuwaweka sawa baada ya mchezo wa Jumamosi ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Kwa sasa tunaelekeza nguvu katika mchezo dhidi ya Coastal kuhakikisha tunapata alama tatu nyumbani.

Wachezaji wapo tayari kuanza programu ya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kuelekea mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Uhuru saa 10 jioni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER