Timu yawasili salama Berkane

Timu yetu imewasili salama katika Mji wa Berkane kutoka jiji la Casablanca tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigiwa Uwanja wa Manispaa wa Berkane saa nne usiku kwa saa za nyumbani.

Baada ya kufika kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane saa nne usiku muda ambao mchezo utapigwa kesho.

Hali ya hewa nchini Morocco ni baridi hasa nyakati za usiku lakini wachezaji wameendelea kuzoea mazingira ili isiwe changamoto kubwa katika mchezo kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER