Kikosi cha wachezaji 23 kimewasili salama mkoani Mtwara tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC utakaopigwa Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.
Baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Mtwara kikosi kimepata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuwalaki wachezaji.
Tunaamini mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani ingawa tutahakikisha tunapambana kurudi na alama zote tatu jijini Dar es Salaam.
Lengo letu ni kukusanya alama tatu katika kila mchezo tutakaocheza kuanzia sasa kwa kuwa bado hatujakata tamaa ya kutetea ubingwa wetu.