Timu yatua salama Marrakech

Kikosi chetu kimewasili salama katika mji wa Marrakech nchini Morocco tayari kwa mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaopigwa Jumamosi saa nne usiku.

Timu iliondoka jijini Dar es Salaam jana mchana ambapo ilipitia Doha Qatar na baadae Casablanca kabla ya kuunganisha hadi Marrakech.

Baada ya timu kufika Marrakhech wachezaji watapewa muda wa kupumzika kutokana na uchovu wa safari kabla ya kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili.

Kikosi kimewasili mapema nchini Morocco ambapo kitapata muda wa siku mbili kufanya mazoezi ambapo wachezaji wataizoea hali ya hewa ili Jumamosi wasipate changamoto yoyote.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER