Timu yatua salama Botswana

Kikosi chetu kimewasili salama nchini Botswana tayari kwa mchezo wa kesho wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa saa 10 jioni katika Uwanja wa Obedi Itani Chilume.

Kikosi kimetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa PG MATANTE katika mji wa Francistown baada ya safari ya masaa matano ya kuwa angani kutoka jijini Dar es Salaam.

Timu inatarajia kufanya mazoezi katika Uwanja wa Obedi Itani ambao tutautumia kwenye mchezo wa kesho kama kanuni za Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) zinavyoelekeza.

Tumeondoka na kikosi cha wachezaji 20 ambao tunaamini watatuwezesha kupata ushindi katika mchezo wa kesho.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER