Timu yarejea salama Dar, wachezaji wapewa mapumziko

Kikosi chetu kimerejea salama jijini Dar es Salaam kutoka Morocco baada ya kumaliza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Baada ya kufika wachezaji wamepewa mapumziko na watarudi mazoezini Jumanne kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ihefu.

Mchezo wetu wa robo fainali dhidi ya Ihefu utapigwa Ijumaa, Aprili 7 saa 10 jioni katika Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo tunaupa umuhimu mkubwa kwakuwa lengo letu ni kuhakikisha tunashinda taji hili kwahiyo tunapaswa kushinda kila mechi ili kufanikisha hilo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER