Timu yarejea salama Dar

Kikosi chetu kimewasili salama jijini Dar es Salaam alfajiri kutoka nchini Guinea baada ya kumalizia mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya FC.

Baada ya kufika wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja na kesho wataanza mazoezi na kuingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo wa pili dhidi ya Raja Casablanca.

Mchezo dhidi ya Raja ambao utapigwa Jumamosi, Februari 18 Uwanja wa Benjamin Mkapa ni muhimu kwetu kupata ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa Kundi C.

Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote za nyumbani na mchezo wa kwanza utakuwa dhidi ya Raja siku Jumamosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER